Surat Fussilat, aya 22

41:22

وَمَا كُنتُمۡ تَسۡتَتِرُونَ أَن يَشۡهَدَ عَلَيۡكُمۡ سَمۡعُكُمۡ وَلَآ أَبۡصَٰرُكُمۡ وَلَا جُلُودُكُمۡ وَلَٰكِن ظَنَنتُمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَا يَعۡلَمُ كَثِيرٗا مِّمَّا تَعۡمَلُونَ ٢٢

Wamā kuntum tastatirūna an yashhada 'alaykum sam'ukum walā absārukum walā julūdukum walākin zanantum annallāha lā ya'lamu kathīram mimmā ta'malūn

Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika mliyo kuwa mkiyatenda. 22

Maelezo ya chini

22 Wala nyinyi hamkuwa mkiweza kuficha vitendo vyenu viovu hata viungo vyenu visivione na ikawa macho yenu, na masikio yenu na ngozi zenu, vyote hivyo vikakushuhudilieni. Lakini nyinyi mlikuwa mkidhani kuwa Mwenyezi Mungu hajui mengi katika vitendo vyenu, kwa sababu mkivifanya kwa uficho.