Surat Fussilat, aya 21

41:21

وَقَالُواْ لِجُلُودِهِمۡ لِمَ شَهِدتُّمۡ عَلَيۡنَاۖ قَالُوٓاْ أَنطَقَنَا ٱللَّهُ ٱلَّذِيٓ أَنطَقَ كُلَّ شَيۡءٖۚ وَهُوَ خَلَقَكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٢١

Waqālū lijulūdihim lima shahittum 'alaynā qālū antaqanallāhul-ladhī antaqa kulla shay'in wahuwa khalaqakum awwala marratin wa ilayhi turja'ūn

Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliye kuumbeni mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa. 21

Maelezo ya chini

21 Na hao maadui wa Mwenyezi Mungu wakaziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Na ngozi zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu aliye tamkisha kila kitu. Na Yeye ndiye aliye kuumbeni hapo mwanzo kabla hamjawa chochote. Na kwake Yeye, peke yake, ndio mtarejea baada ya kufufuliwa, akuhisabieni mliyo kwisha yatanguliza katika vitendo.