Surat Fatir, aya 44

35:44

أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَكَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعۡجِزَهُۥ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمٗا قَدِيرٗا ٤٤

Awalam yasīrū fil-ardi fayanzurū kayfa kāna 'āqibatul-ladhīna min qablihim wakānū ashadda minhum quwwatan wamā kānallāhu liyu'jizahū min shay'in fis-samāwāti walā fil-ardi innahū kāna 'alīman qadīrā

Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uweza. 44

Maelezo ya chini

44 Je! hao hukaa na wakakanya tu ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina, bila ya wao kusafiri katika ulimwengu wakaangalia kwa macho yao athari za maangamizo yaliyo wateremkia walio kuwa kabla yao kwa sababu ya kuwakadhibisha kwao Mitume? Na kabla ya wao yalikuwako mataifa yaliyo kuwa na nguvu kushinda wao. Nguvu zao hazikuweza kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye hashindwi na chochote kilioko mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye ilimu kubwa kabisa, Mwenye uweza mkubwa kabisa.