Surat Fatir, aya 45

35:45

وَلَوۡ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُواْ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهۡرِهَا مِن دَآبَّةٖ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗىۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرَۢا ٤٥

Walaw yu'ākhidhullāhun-nāsa bimā kasabū mā taraka 'alā zahrihā min dābbatin walākin yu'akkhiruhum ilā ajalim musamman fa idhā jā'a ajaluhum fa innallāha kāna bi'ibādihī basīrā

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara. 45

Maelezo ya chini

45 Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli kuwa anawaadhibu watu duniani, basi hapana shaka adhabu yake ingeli enea. Na asingeli muacha juu ya mgongo wa ardhi hata mnyama mmoja, kwa kuwa wote wametenda madhambi. Lakini anaakhirisha kuwaadhibu mpaka siku maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama. Basi ukifika muda wao walio wekewa atawalipa kwa uangalizi kaamili. Kwani Yeye ni Mwenye kuviona vitendo vya waja wake; hafichikiwi na kitu chochote katika hivyo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua kushinda wote.