Surat Az-Zumar, aya 69

39:69

وَأَشۡرَقَتِ ٱلۡأَرۡضُ بِنُورِ رَبِّهَا وَوُضِعَ ٱلۡكِتَٰبُ وَجِاْيٓءَ بِٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡحَقِّ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ ٦٩

Wa ashraqatil-ardu binūri rabbihā wawudi'al-kitābu wajiy'a bin-nabiyyina wash-shuhadā'i waqudiya baynahum bil-haqqi wahum lā yuzlamūn

Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. 69

Maelezo ya chini

69 Na ardhi itang'ara siku hiyo kwa nuru ya Muumba wake na Mmiliki wake. Na kitatayarishwa Kitabu kilicho sajiliwa ndani yake vitendo vyao, na watahudhurishwa Manabii na mashahidi wapate kuwashuhudia viumbe vyote, na wapambanuliwe baina ya viumbe kwa uadilifu, na wala hawatadhulumiwa kwa kupunguziwa thawabu wala kuzidishiwa adhabu.