وَتَبَارَكَ ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ ٨٥
Watabārakal-ladhī lahū mulkus-samāwāti wal-ardi wamā baynahumā wa'indahū 'ilmus-sā'ati wa ilayhi turja'ūn
Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa. 85
Maelezo ya chini
85 Na ametukuka na ametaadhamu Yeye ambaye, peke yake, Mwenye ukamilifu wa kutekeleza katika mbingu na ardhi na baina yao katika viumbe vya angani vinavyo onekana na vyenginevyo, na mipango yote iko kwake, na Yeye tu ndiye Mwenye kujua wakati wa Kiyama, na kwake Yeye peke yake, mtarejeshwa mwishoe kwa ajili ya hisabu.