Surat Az-Zukhruf, aya 84

43:84

وَهُوَ ٱلَّذِي فِي ٱلسَّمَآءِ إِلَٰهٞ وَفِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَٰهٞۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ ٨٤

Wahuwal-ladhī fis-samā'i ilāhun wafil-ardi ilāhun wahuwal-hakīmul-'alīm

Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hikima, Mwenye ujuzi. 84

Maelezo ya chini

84 Na Yeye ndiye anaye abudiwa mbinguni kwa haki, na anaabudiwa katika ardhi kwa haki. Na Yeye, peke yake, ndiye Mwenye hikima za mwisho katika vitendo vyake na mipango yake, Mwenye kujua kila kitu kilicho kuwa na kitakacho kuwa.