Surat Az-Zukhruf, aya 48

43:48

وَمَا نُرِيهِم مِّنۡ ءَايَةٍ إِلَّا هِيَ أَكۡبَرُ مِنۡ أُخۡتِهَاۖ وَأَخَذۡنَٰهُم بِٱلۡعَذَابِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ ٤٨

Wamā nurīhim min āyatin illā hiya akbaru min ukhtihā wa akhadhnāhum bil-'adhābi la'allahum yarji'ūn

Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee. 48

Maelezo ya chini

48 Na kila muujiza katika miujiza iliyo wajia mfululizo, kwa uwazi wa hoja zake juu ya ukweli wa Mtume, na kuwa kila mmoja peke yake unatimiza makusudio hayo kwa ukamilifu wa kila njia, na ukamilifu wa nafsi yake, hata ukiuangalia waweza kusema: Muujiza huu ni mkubwa kuliko ule mwengine. Na walipo shikilia kuendelea na uasi tuliwapatiliza kwa balaa za namna kwa namna, ili warejee, waache upotovu wao.