وَقَالُواْ يَٰٓأَيُّهَ ٱلسَّاحِرُ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهۡتَدُونَ ٤٩
Waqālū yā'ayyuhas-sāhirud'u lanā rabbaka bimā 'ahida 'indaka innanā lamuhtadūn
Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka. 49
Maelezo ya chini
49 Wakasema, kumlilia Musa balaa zilipo waenea: Ewe mchawi - ndio Mwanachuoni kikwao - Tuombee kwa Mola wako Mlezi, kwa kutawasali na ahadi yake aliyo kupa, atuondolee adhabu hii! Hakika sisi tukifarijiwa bila ya shaka tutaongoka.