فَذَكِّرۡ فَمَآ أَنتَ بِنِعۡمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٖ وَلَا مَجۡنُونٍ ٢٩
Fadhakkir famā anta bini'mati rabbika bikāhinin walā majnūn
Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. 29
Maelezo ya chini
29 Wewe endelea na kukumbusha kama unavyo fanya. Kwani wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu aliyo kuneemesha kukupa Unabii na akili iliyo timia, si kuhani anaye toa khabari za ghaibu bila ya ilimu, wala si mwendawazimu unaye sema usiyo yasadiki.