Surat At-Tawbah, aya 87

9:87

رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ ٨٧

Radū bi an yakūnū ma'al-khawālifi watubi'a 'alā qulūbihim fahum lā yafqahūn

Wameridhia kuwa pamoja na wabakiao nyuma, na nyoyo zao zikapigwa muhuri; kwa hivyo hawafahamu. 87

Maelezo ya chini

87 Hao hakika wamejikubalia wenyewe wahisabike katika walio bakia nyuma, nao ni wanawake, na wasio jiweza, na watoto wadogo wasio viweza vita. Na Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao kwa khofu na unaafiki. Basi hao hawafahamu vilivyo uhakika wa Jihadi na kumfuata Mtume, nako ni kupata utukufu duniani na kupata radhi ya Mwenyezi Mungu katika Akhera.