وَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٌ أَنۡ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَجَٰهِدُواْ مَعَ رَسُولِهِ ٱسۡتَـٔۡذَنَكَ أُوْلُواْ ٱلطَّوۡلِ مِنۡهُمۡ وَقَالُواْ ذَرۡنَا نَكُن مَّعَ ٱلۡقَٰعِدِينَ ٨٦
Wa idhā unzilat sūratun an āminū billāhi wajāhidū ma'a rasūlihista'dhanaka ulut-tawli minhum waqālū dharnā nakum ma'al-qā'idīn
Na inapo teremshwa Sura isemayo: Muaminini Mwenyezi Mungu na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye nguvu miongoni mwao hukutaka ruhusa na husema: Tuache tuwe pamoja na wanao kaa nyuma! 86
Maelezo ya chini
86 Na hawa wanaafiki wakisikia chochote ulicho teremshiwa katika Qur'ani kinacho wataka wamsafie Imani Mwenyezi Mungu, na wende kwenye Jihadi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, matajiri na wenye nguvu katika wao wanakutaka uwaachilie wasende nawe kwenye Jihadi, na husema: Tuache tuwe na hawa walio pewa ruhusa kukaa nyuma Madina.