Surat At-Tawbah, aya 88

9:88

لَٰكِنِ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ جَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡخَيۡرَٰتُۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ٨٨

Lākinir-rasūlu walladhīna āmanū ma'ahū jāhadū bi amwālihim wa anfusihim wa ulā'ika lahumul-khayrātu wa ulā'ika humul-muflihūn

Lakini Mtume na wale walio amini pamoja naye waliwania Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa. 88

Maelezo ya chini

88 Hiyo ndiyo hali ya wanaafiki. Lakini Mtume na wale walio sadiki pamoja naye, wametoa mali zao na roho zao ili kumridhi Mwenyezi Mungu, na kulinyanyua Neno lake. Hao tu peke yao ndio watakao pata kila kheri ya duniani, nayo ni utukufu na ushindi, na a'mali njema. Na wao peke yao ndio wenye kufuzu.