وَمَا مَنَعَهُمۡ أَن تُقۡبَلَ مِنۡهُمۡ نَفَقَٰتُهُمۡ إِلَّآ أَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأۡتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمۡ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمۡ كَٰرِهُونَ ٥٤
Wamā mana'ahum an tuqbala minhum nafaqātuhum illā annahum kafarū billāhi wabirasūlihī walā ya'tūnas-salawāta illā wahum kusālā walā yunfiqūna illā wahum kārihūn
Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala hawatoi michango ila nao wamechukia. 54
Maelezo ya chini
54 Wala Mwenyezi Mungu hakukataza visipokelewe wanavyo vitoa ila kwa kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ukafiri, kukataa, kunavunja a'mali zote. Na vile kwa kuwa wao hawaswali kwa namna walio amrishwa; kwani wao huswali bila ya kuiamini Swala, ila wanafanya kama ni kuficha unaafiki wao. Wala wao hawatoi kitu isipo kuwa na huku wanachukia huko kutoa ndani ya nyoyo zao.