قُلۡ أَنفِقُواْ طَوۡعًا أَوۡ كَرۡهٗا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمۡ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ ٥٣
Qul anfiqū taw'an aw karhal lan yutaqabbala minkum innakum kuntum qawman fāsiqīn
Sema: Toeni mkipenda msipende. Hakitopokelewa kitu kwenu, kwani nyinyi ni watu wapotovu. 53
Maelezo ya chini
53 Ewe Mtume! Waambie hao wanaafiki wanao taka kuficha unaafiki wao kwa kutoa michango ya mali kwa ajili ya Jihadi na mengineyo: Toeni mtakacho, kwa khiari au kwa nguvu; Mwenyezi Mungu havikubali vitendo vyenu vilivyo kwisha haribiwa na unaafiki wenu! Kwani nyinyi daima ni wenye kuiasi Dini ya Mwenyezi Mungu, wenye kuipinga amri yake.