قُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٥١
Qul lan yusībanā illā mā kataballāhu lanā huwa mawlānā wa'alallāhi falyatawakkalil-mu'minūn
Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu! 51
Maelezo ya chini
51 Waambie ewe Mtume: Hayatupati ya kheri wala ya shari katika hii dunia yetu, ila aliyo tukadiria Mwenyezi Mungu. Kwani sisi turadhi na hukumu ya Mwenyezi Mungu. Hatujitapi kwa kheri, wala hatuingiwi na dukuduku la roho kwa kufikiwa na shari. Hakika Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kuyatawala mambo yetu yote, na juu yake Yeye tu ndio Waumini wa kweli wanategemea.