Surat At-Tawbah, aya 50

9:50

إِن تُصِبۡكَ حَسَنَةٞ تَسُؤۡهُمۡۖ وَإِن تُصِبۡكَ مُصِيبَةٞ يَقُولُواْ قَدۡ أَخَذۡنَآ أَمۡرَنَا مِن قَبۡلُ وَيَتَوَلَّواْ وَّهُمۡ فَرِحُونَ ٥٠

In tusibka hasanatun tasu'hum wa in tusibka musībatun yaqūlū qad akhadhnā amranā min qablu wayatawallaw wwahum farihūn

Ukikupata wema unawachukiza, na ukikusibu msiba, wao husema: Sisi tuliangalia mambo yetu vizuri tangu kwanza. Na hugeuka kwenda zao nao wamefurahi. 50

Maelezo ya chini

50 Hawa wanaafiki hawakutakii wewe Mtume na Masahaba zako ila mambo ya karaha tu. Wanaona uchungu mkipata kheri yoyote, ikiwa ya ushindi au ngawira; na wanafurahi mkisibiwa na shari, kama kujeruhiwa au kuuwawa! Na yakikupateni hayo wao husema kwa kufurahia msiba wenu: Sisi tulichukua hadhari yetu, kwa kubaki nyuma tusitoke kwenda kwenye Jihadi. Na huenda zao nao wamefurahi.