يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَا لَكُمۡ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلۡتُمۡ إِلَى ٱلۡأَرۡضِۚ أَرَضِيتُم بِٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ فَمَا مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ ٣٨
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū mā lakum idhā qīla lakumunfirū fī sabīlillāhit-thāqaltum ilal-ardi aradītum bil-hayawātid-dunyā minal-ākhirati famā matā'ul-hayawātid-dunyā fil-ākhirati illā qalīl
Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. 38
Maelezo ya chini
38 Enyi Waumini! Mna nini, anapo kwambieni Mtume: Tokeni mwende kwenye Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baadhi yenu mkafanya uzito kutoka? Haikufalieni hivyo! Mnaona afadhali maisha ya dunia yatayo kwisha, kuliko maisha ya Akhera na neema zake za kudumu? Starehe ya duniani na utamu wake ukilinganisha na starehe ya Akhera ni chache na upuuzi.