Surat At-Tawbah, aya 37

9:37

إِنَّمَا ٱلنَّسِيٓءُ زِيَادَةٞ فِي ٱلۡكُفۡرِۖ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُحِلُّونَهُۥ عَامٗا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامٗا لِّيُوَاطِـُٔواْ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّواْ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُۚ زُيِّنَ لَهُمۡ سُوٓءُ أَعۡمَٰلِهِمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡكَٰفِرِينَ ٣٧

Innaman-nasī'u ziyādatun fil-kufri yudallu bihil-ladhīna kafarū yuhillūnahū 'āman wayuharrimūnahū 'āmal liyuwāti'ū 'iddata mā harramallāhu fayuhillū mā harramallāhu zuyyina lahum sū'u a'mālihim wallāhu lā yahdil-qawmal-kāfirīn

Bila ya shaka kuakhirisha (miezi) ni kuzidi katika kukufuru; kwa hayo hupotezwa walio kufuru. Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharimisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyo itukuza Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo huhalalisha alivyo viharimisha Mwenyezi Mungu. Wamepambiwa ubaya wa vitendo vyao hivi. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri. 37

Maelezo ya chini

37 Na hakukuwa kuichelewesha miezi mitakatifu, au baadhi yake, kuliko alivyo iweka Mwenyezi Mungu, ila ni kuzidi ukafiri, kama walivyo kuwa wakifanya watu wa kijahiliya. Hao makafiri wakizidisha hivyo kuongeza upotovu juu ya upotovu! Waarabu wakati wa ujuhali walikuwa hufanya mwezi uliyo harimishwa kupigana vita kuwa ni wa halali, pindi wakihitajia kupigana. Na hufanya mwezi ulio halalishwa ndio ulio harimishwa. Na wakisema: Mwezi kwa mwezi. Yaani kulipizia ipate kutimia idadi ile aliyo harimisha Mwenyezi Mungu. Matamanio yao yamewapendezeshea kitendo chao hicho kiovu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu walio shikilia kukataa kuifuata Njia ya kwendea Kheri.