۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡأَحۡبَارِ وَٱلرُّهۡبَانِ لَيَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۗ وَٱلَّذِينَ يَكۡنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلۡفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٖ ٣٤
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū inna kathīram minal-ahbāri war-ruhbāni laya'kulūna amwālan-nāsi bil-bātili wayasuddūna 'an sabīlillāhi walladhīna yaknizūnadh-dhahaba wal-fiddata walā yunfiqūnahā fī sabīlillāhi fabasshirhum bi'adhābin alīm
Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat'ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu. 34
Maelezo ya chini
34 Enyi Waumini! Jueni kuwa wengi katika wataalamu wa Kiyahudi na mapadri wa Kikristo wanajihalalishia kula mali ya watu bila ya haki yoyote, na wanawazuga wafwasi wao wanao waamini kwa kila walisemalo. Na wanawazuilia watu wasiingie katika Uislamu. Na wale wanao kusanya mali, dhahabu na fedha, wakiyaweka tu, wala hawatoi Zaka zake, waonye ewe Mtume, kuwa kuna adhabu ya kutia uchungu _