Surat At-Tawbah, aya 28

9:28

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡمُشۡرِكُونَ نَجَسٞ فَلَا يَقۡرَبُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ ٱلۡحَرَامَ بَعۡدَ عَامِهِمۡ هَٰذَاۚ وَإِنۡ خِفۡتُمۡ عَيۡلَةٗ فَسَوۡفَ يُغۡنِيكُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦٓ إِن شَآءَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ٢٨

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū innamal-mushrikūna najasun falā yaqrabul-masjidal-harāma ba'da 'āmihim hādhā wa in khiftum 'aylatan fasawfa yughnīkumullāhu min fadlihī in shā'a innallāha 'alīmun hakīm

Enyi mlio amini! Hakika washirikina ni najsi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu. Na ikiwa mnakhofia umasikini, basi Mwenyezi Mungu atakutajirisheni kwa fadhila yake akipenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. 28

Maelezo ya chini

28 Enyi Waumini! Washirikina kwa sababu ya ushirikina wao wamejinajisi nafsi zao, nao wamepotea katika itikadi. Msiwaachilie kuingia Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka huu (9 Hijra). Mkichelea ufakiri kwa kukatika biashara Mwenyezi Mungu atakupeni badala yake, na atakutoshelezeni kwa fadhila yake akipenda. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua mambo yenu yote, na Mwenye hikima katika mipango yake.