Surat At-Tawbah, aya 21

9:21

يُبَشِّرُهُمۡ رَبُّهُم بِرَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَرِضۡوَٰنٖ وَجَنَّٰتٖ لَّهُمۡ فِيهَا نَعِيمٞ مُّقِيمٌ ٢١

Yubasshiruhum rabbuhum birahmatim minhu waridwānin wajannātil lahum fīhā na'īmum muqīm

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. 21

Maelezo ya chini

21 Na hao Mwenyezi Mungu Mtukufu anawabashiria rehema kunjufu itakayo waenea, na atawakhusisha radhi zake, na hayo ndiyo malipo makuu. Na Siku ya Kiyama atawatia katika Mabustani, na humo watapata neema zenye kuthibiti na kudumu.