Surat At-Tawbah, aya 110

9:110

لَا يَزَالُ بُنۡيَٰنُهُمُ ٱلَّذِي بَنَوۡاْ رِيبَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ١١٠

Lā yazālu bunyānuhumul-ladhī banaw rībatan fī qulūbihim illā an taqatta'a qulūbuhum wallāhu 'alīmun hakīm

Na jengo lao hilo walilo lijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. 110

Maelezo ya chini

110 Na hilo jengo lao walilo lijenga wanaafiki litakuwa ni sababu ya kuwakereketa na kuwatia khofu katika nyoyo zao. Hayeshi hayo mpaka zipasuke nyoyo zao kwa majuto na kutubu au wafe! Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, na Mwenye hikima katika vitendo vyake na malipo yake.