وَءَاخَرُونَ مُرۡجَوۡنَ لِأَمۡرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمۡ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيۡهِمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ١٠٦
Wa ākharūna murjawna li amrillāhi immā yu'addhibuhum wa immā yatūbu 'alayhim wallāhu 'alīmun hakīm
Na wapo wengine wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu - ama atawaadhibu au atawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. 106
Maelezo ya chini
106 Na wapo watu wengine wametumbukia katika madhambi - wameacha kwenda kwenye Jihadi, lakini hawana unaafiki. Watu hawa wanangojea amri ya Mwenyezi Mungu. Ama awaadhibu au awakubalie toba yao awasamehe. Na Mwenyezi Mungu anazijua hali zao, na yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Naye ni Mwenye hikima kwa ayafanyayo kwa waja wake, ikiwa kuwalipa thawabu au adhabu.