Surat At-Tawbah, aya 101

9:101

وَمِمَّنۡ حَوۡلَكُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مُنَٰفِقُونَۖ وَمِنۡ أَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ مَرَدُواْ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعۡلَمُهُمۡۖ نَحۡنُ نَعۡلَمُهُمۡۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيۡنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٖ ١٠١

Wamimman hawlakum minal-a'rābi munāfiqūna wamin ahlil-madīnati maradū 'alan-nifāqi lā ta'lamuhum nahnu na'lamuhum sanu'addhibuhum marratayni thumma yuraddūna ilā 'adhābin 'azīm

Na katika mabedui walio jirani zenu wamo wanaafiki; na katika wenyeji wa Madina pia wapo walio bobea katika unaafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa. 101

Maelezo ya chini

101 Na katika walio kuwa jirani na Madina miongoni mwa watu wa majangwani, walikuwako walio kuwa wakificha ukafiri wao na wakijidhihirisha kuwa ni Waumini. Na katika wakaazi wa Madina walikuwapo walio kuwa wamezoea unaafiki hata wakawa mabingwa, na wakawa wanauficha watu wasiutambue! Hata mwisho wewe, Mtume, usiwajue. Lakini Mwenyezi Mungu anajua hakika yao, na atawaadhibu duniani mara mbili - mara ya kwanza kwa kuwashinda maadui zenu, na hayo yatawaudhi wao; na mara nyingine kwa kuwafedhehi na kuwakashifu unaafiki wao. Tena, basi, watarejeshwa Siku ya Akhera kwenye adhabu ya Moto, na vitisho vyake vikubwa.