وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلۡأَوَّلُونَ مِنَ ٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ وَٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُم بِإِحۡسَٰنٖ رَّضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي تَحۡتَهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ١٠٠
Was-sābiqūnal-awwalūna minal-muhājirīna wal-ansāri walladhīnat-taba'ūhum bi ihsānir radiyallāhu 'anhum waradū 'anhu wa a'adda lahum jannātin tajrī tahtahal-anhāru khālidīna fīhā abadan dhālikal-fawzul-'azīm
Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 100
Maelezo ya chini
100 Na Waumini walio tangulia kusilimu, na Wahajiri (walio hama Makka kwenda Madina) na Ansari (wasaidizi wa Madina walio wapokea) walio kwenda mwendo mzuri wala hawakufanya taksiri, Mwenyezi Mungu yu radhi nao. Basi anawapokea na anawalipa mema. Na wao kadhaalika wameridhika na wamefurahia aliyo waandalia Mwenyezi Mungu, nayo ni Mabustani yapitayo mito kati ya miti yake. Wataneemeka humo kwa neema ya milele. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.