Surat At-Taghabun, aya 11

64:11

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ يَهۡدِ قَلۡبَهُۥۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ ١١

Mā asāba mim musībatin illā bi idhnillāhi waman yu'mim billāhi yahdi qalbahū wallāhu bikulli shay'in 'alīm

Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. 11

Maelezo ya chini

11 Mja hasibiwi na balaa ila kwa kudra ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumsadiki Mwenyezi Mungu basi humwongoa moyo wake kwendea katika yanayo mpendeza. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimia ujuzi wake.