وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَۚ فَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ ١٢
Wa atī'ullāha wa atī'ur-rasūla fa in tawallaytum fa innamā 'alā rasūlinal-balāghul-mubīn
Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu. 12
Maelezo ya chini
12 Na mt'iini Mwenyezi Mungu kwa aliyo kuamrisheni, na mt'iini Mtume kwa Ujumbe aliyo kufikishieni kutoka kwa Mola wake Mlezi. Mkiupuuza ut'iifu huu, basi Yeye hadhuriki kitu kwa mapuuza yenu. Na hakika Mtume wetu hana jukumu juu yake ila kufikisha Utume wake tu kwa uwazi.