وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ ٣١
Wamā antum bimu'jizīna fil-ardi wamā lakum min dūnillāhi min waliyyin walā nasīr
Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu. 31
Maelezo ya chini
31 Wala nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu na kumzuilia asilete masaibu duniani kuwa ni adhabu kwa ajili ya maasi yenu, na hata mkikimbia vipi. Na wala hamna asiye kuwa Mwenyezi Mungu wa kukurehemuni pindi ikikuteremkieni balaa, wala hamna wa kukunusuruni nayo.