لَهُۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُۚ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ ١٢
Lahū maqālīdus-samāwāti wal-ardi yabsutur-rizqa liman yashā'u wayaqdiru innahū bikulli shay'in 'alīm
Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. 12
Maelezo ya chini
12 Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi, kwa kuzihifadhi na kuzitumia. Humkunjulia riziki amtakaye, na humdhikisha amtakaye. Hakika Yeye, Mtukufu, ujuzi wake umezunguka kila kitu.