فَاطِرُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ جَعَلَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٰجٗا وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ أَزۡوَٰجٗا يَذۡرَؤُكُمۡ فِيهِۚ لَيۡسَ كَمِثۡلِهِۦ شَيۡءٞۖ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ ١١
Fātirus-samāwāti wal-ardi ja'ala lakum min anfusikum azwājan waminal-an'āmi azwājan yadhra'ukum fīhi laysa kamithlihī shay'un wahuwas-samī'ul-basīr
Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. 11
Maelezo ya chini
11 Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuumbieni katika jinsi yenu wanaume na wanawake, na akaumba katika mifugo yenu kadhaalika madume na majike, na kwa mpango huu ndio wazidi kuwa wengi. Hapana kitu chochote kama mfano wake Mwenyezi Mungu, basi hana kitu cha kuwa wa pili yake. Na Yeye ndiye Mwenye kujua, kwa ujuzi wa kukamilika, kuvijua vyote vinavyo sikilizana na kuonekana bila ya taathira ya hisiya.