قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُۥ بُنۡيَٰنٗا فَأَلۡقُوهُ فِي ٱلۡجَحِيمِ ٩٧
Qālubnū lahū bunyānan fa alqūhu fil-jahīm
Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo! 97
Maelezo ya chini
97 Hoja ilipo wapata wale wanao abudu masanamu, wakaona hawana ila waingie kutumia nguvu; wakaazimia kumchoma moto. Basi waliambizana: Mjengeeni jengo, na mlijaze moto, na mtupeni katikati yake!