وَعِندَهُمۡ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ عِينٞ ٤٨
Wa'indahum qāsirātut-tarfi 'īn
Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. 48
Maelezo ya chini
48 Na watu hawa wat'iifu walioko Peponi watakuwa nao mahuruleini walio safi, wema, macho yao hayawatazami ila waume zao tu, basi hawayatafuti matamanio maovu, jicho la mwema haliangalii ila mema.