Surat As-Saffat, aya 141

37:141

فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُدۡحَضِينَ ١٤١

Fasāhama fakāna minal-mudhadīn

Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa. 141

Maelezo ya chini

141 Alipo wahama watu wake bila ya amri ya Mola wake Mlezi, akaliendea jahazi ambalo lilio kwisha sheheni pomoni, akalipanda. Jahazi likapatikana na mambo ikawajibikia lazima mmoja katika abiria atoswe kupunguza shehena yake. Kura ikamuangukia Yunus, akashindwa kwa kura. Akatoswa baharini kwa mujibu wa ada yao zama zile.