وَبَشَّرۡنَٰهُ بِإِسۡحَٰقَ نَبِيّٗا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ١١٢
Wabassharnāhu bi ishāqa nabiyyam minas-sālihīn
Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema. 112
Maelezo ya chini
112 Na kwa amri yetu, Malaika walimbashiria kuwa ataruzukiwa mwana, Is-haqa juu ya kukata tamaa na kuwa mkewe ni tasa. Na kwamba yeye hakika atakuwa Nabii miongoni mwa walio wema.