Surat Ar-Ra'd, aya 5

13:5

۞ وَإِن تَعۡجَبۡ فَعَجَبٞ قَوۡلُهُمۡ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا أَءِنَّا لَفِي خَلۡقٖ جَدِيدٍۗ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡأَغۡلَٰلُ فِيٓ أَعۡنَاقِهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ٥

Wa in ta'jab fa'ajabun qawluhum a'idhā kunnā turāban a'innā lafī khalqin jadīdin ulā'ikal-ladhīna kafarū birabbihim wa ulā'ikal-aghlālu fī a'nāqihim wa ulā'ika ashābun-nāri hum fīhā khālidūn

Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Ati tukisha kuwa mchanga kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio walio mkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watao kuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu. 5

Maelezo ya chini

5 Na hakika mambo ya washirikina juu ya dalili hizi ni ya ajabu. Ikiwa wewe Muhammad utas- taajabia jambo, basi la ajabu ni hiyo kauli yao wanapo sema: Ati baada ya kufa, na baada ya kwisha kuwa mchanga, tutakuwa wahai tena upya? Huu ndio mtindo wa wanao mkufuru Muumba wao. Akili zao zimefungwa na upotovu. Na marejeo yao ni Motoni watakapo dumu humo; kwani hao ni wenye kukanya juu ya kuwa mwenye kuweza kuanzisha anaweza kurejesha.