ٱلَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَلَا يَنقُضُونَ ٱلۡمِيثَٰقَ ٢٠
Alladhīna yūfūna bi'ahdillāhi walā yanqudūnal-mīthāq
Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji maagano. 20
Maelezo ya chini
20 Hao ndio wanao tambua Haki. Wao ndio wanao timiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyo juu yao kwa muujibu wa maumbile, na kwa muujibu wa maagano yao na ahadi zao walizo fungamana nazo; wala hawavunji maagano walio fungamana nayo kwa jina la Mwenyezi Mungu baina yao na waja wenzi wao, na kwa maagano makubwa walio jifunga nayo kwa maumbile yaliyo wafanya waitambue Haki na waamini, isipo kuwa walipo jipoteza wenyewe nafsi zao.