وَٱلَّذِينَ يَصِلُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيَخۡشَوۡنَ رَبَّهُمۡ وَيَخَافُونَ سُوٓءَ ٱلۡحِسَابِ ٢١
Walladhīna yasilūna mā amarallāhu bihī an yūsala wayakhshawna rabbahum wayakhāfūna sū'al-hisāb
Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya. 21
Maelezo ya chini
21 Hao ni Waumini; ada yao ni mapenzi na ut'iifu. Hao wanaamini mapendo baina ya watu, na wanahurumia jamaa zao, na wanawasaidia wenzi wao katika Haki, na wao wanaijua Haki ya Mwenyezi Mungu, na wanaiogopa hisabu ya kuwachusha Siku ya Kiyama, na kwa hivyo wanajikinga na madhambi kwa kadri wawezavyo.