لِلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِرَبِّهِمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱلَّذِينَ لَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُۥ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ سُوٓءُ ٱلۡحِسَابِ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ ١٨
Lilladhīnastajābū lirabbihimul-husnā walladhīna lam yastajībū lahū law anna lahum mā fil-ardi jamī'an wamithlahū ma'ahū laftadaw bihī ulā'ika lahum sū'ul-hisābi wama'wāhum jahannamu wabi'sal-mihād
Walio muitikia Mola wao Mlezi watapata wema. Na wasio muitikia, hata wangeli kuwa navyo vyote viliomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikombolea! Hao watapata hisabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahala pabaya mno! 18
Maelezo ya chini
18 Watu kwa mujibu wa kupokea kwao uwongofu ni mafungu mawili. Fungu moja lilio itikia wito wa Mwenyezi Mungu Muumba Mwenye kupanga. Hilo litapata malipo mema duniani na Akhera. Fungu jengine lisilo itikia wito wa Aliye waumba. Hawa watapata malipo maovu Akhera. Na lau kuwa wanamiliki kila kiliomo duniani na mfano wake mara ya pili, hawawezi kujikinga na hayo malipo maovu! Lakini watapata kumiliki hayo? Kwa hivyo yao wao ni hisabu ya kuwaudhi, na wataishia katika Jahannamu, na huko ni pahali paovu mno pa kuishi.