Surat An-Nur, aya 51

24:51

إِنَّمَا كَانَ قَوۡلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ إِذَا دُعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحۡكُمَ بَيۡنَهُمۡ أَن يَقُولُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ ٥١

Innamā kāna qawlal-mu'minīna idhā du'ū ilallāhi warasūlihī liyahkuma baynahum an yaqūlū sami'nā wa ata'nā wa ulā'ika humul-muflihūn

Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumet'ii! Na hao ndio wenye kufanikiwa. 51

Maelezo ya chini

51 Hakika kauli ya haki ifaayo kwa Waumini wa kweli wanapo itwa wahukumiwe kwa mujibu wa yaliyo kuja kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ni kuwa waseme kwa kukubali na kunyenyekea: Tumesikia wito wako, ewe Muhammad! Na tumeridhia hukumu yako. Na hao ndio watao kuwa watu wa kufanikiwa katika dunia yao na Akhera yao.