Surat An-Nisa, aya 66

4:66

وَلَوۡ أَنَّا كَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ أَنِ ٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ أَوِ ٱخۡرُجُواْ مِن دِيَٰرِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٞ مِّنۡهُمۡۖ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ فَعَلُواْ مَا يُوعَظُونَ بِهِۦ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ وَأَشَدَّ تَثۡبِيتٗا ٦٦

Walaw annā katabnā 'alayhim aniqtulū anfusakum awikhrujū min diyārikum mā fa'alūhu illā qalīlum minhum walaw annahum fa'alū mā yū'azūna bihī lakāna khayral lahum wa ashadda tathbītā

Na lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingeli fanya hayo ila wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeli fanya walio waidhiwa ingeli kuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi. 66

Maelezo ya chini

66 Na lau kuwa Sisi tumewalazimisha mashaka ya mwisho, kwa kuwaamrisha wapigane Jihadi moja kwa moja, na wajitolee nafsi zao kutilifu, au watoke nje waache majumba yao kwenda pigana Jihadi daima, wasinge kubali kut'ii ila wachache tu. Lakini Mwenyezi Mungu, Aliye takasika na kutukuka, hakalifishi ila linalo wezekana. Na lau kuwa wange fanya hayo na wakafuata haki yake ingeli kuwa ni kheri yao ya duniani na Akhera. Na hivyo ndiyo inavyo pelekea kuthibiti Imani, na kuingia imara, na kuleta utulivu.