فَكَيۡفَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ جَآءُوكَ يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّآ إِحۡسَٰنٗا وَتَوۡفِيقًا ٦٢
Fakayfa idhā asābathum musībatu bimā qaddamat aydīhim thumma jā'ūka yahlifūna billāhi in aradnā illā ihsānan watawfīqā
Basi inakuwaje unapo wasibu msiba kwa sababu ya yale iliyo tanguliza mikono yao? Hapo tena hukujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hatukutaka ila wema na mapatano. 62
Maelezo ya chini
62 Itakuwaje hali basi yakiwateremkia masaibu kwa sababu ya uovu wao na upotovu wa vitendo vyao, na wasipate pa kukimbilia ila kwako! Hapo basi watakuapia Mungu mbele yako kuwa wao hawakukusudia kwa maneno yao na vitendo vyao ila wema tu na kutaka mapatano.