Surat An-Nisa, aya 63

4:63

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَعِظۡهُمۡ وَقُل لَّهُمۡ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَوۡلَۢا بَلِيغٗا ٦٣

Ulā'ikal-ladhīna ya'lamullāhu mā fī qulūbihim fa a'rid 'anhum wa'izhum waqul lahum fī anfusihim qawlā balīghā

Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao. 63

Maelezo ya chini

63 Hao ndio wanao kula yamini kuwa hawakutaka ila wema na vitendo vya muwafaka. Mwenyezi Mungu anayajua vyema yaliyomo katika nyoyo zao, na anaujua uwongo wa hiyo kauli yao. Basi wewe usishughulike na maneno yao. Waite kwenye haki kwa mawaidha yaliyo mema, na sema nao maneno yenye hikima yenye kuathiri yanayo fika ndani ya nyoyo zao.