Surat An-Nisa, aya 49

4:49

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُمۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّي مَن يَشَآءُ وَلَا يُظۡلَمُونَ فَتِيلًا ٤٩

Alam tara ilal-ladhīna yuzakkūna anfusahum balillāhu yuzakkī man yashā'u walā yuzlamūna fatīlā

Jee huwaoni wale wanao dai kuwa ati wametakasika? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kadiri ya kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende. 49

Maelezo ya chini

49 Hustaajabii hali ya hao makafiri wanao zua kwa vitendo vyao? Vitendo vyao viovu wao wanaviona kuwa ni vizuri. Wanajisifu kuwa kwa vitendo hivyo wao wametakasika. Na ni Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye anaye jua jema na baya. Yeye ndiye wa kumtakasa amtakaye, na wala hamdhulumu mtu yeyote kadiri yake hata chembe.