Surat An-Nisa, aya 47

4:47

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ ءَامِنُواْ بِمَا نَزَّلۡنَا مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبۡلِ أَن نَّطۡمِسَ وُجُوهٗا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدۡبَارِهَآ أَوۡ نَلۡعَنَهُمۡ كَمَا لَعَنَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلسَّبۡتِۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولًا ٤٧

Yā'ayyuhal-ladhīna ūtul-kitāba āminū bimā nazzalnā musaddiqal limā ma'akum min qabli an natmisa wujūhan fanaruddahā 'alā adbārihā aw nal'anahum kamā la'annā ashābas-sabti wakāna amrullāhi maf'ūlā

Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike. 47

Maelezo ya chini

47 Enyi mlio pewa Kitabu alicho teremsha Mwenyezi Mungu! Iaminini Qur'ani tuliyo mteremshia Muhammad, inayo sadikisha mliyo nayo, kabla hatujawateremshia adhabu ya kufutwa nyuso zenu zikawa kama visogo, hazina pua, wala macho, wala nyusi. Au tukakutoeni katika rehema yetu kama tulivyo watoa wale walio ikhalifu amri yetu wakatenda waliyo katazwa ya kuvua samaki siku ya mapumziko,(Sabt au Sabato) siku ya Jumaamosi. Na hukumu ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutimizwa tu, wala hapana cha kuipinga.