وَمَاذَا عَلَيۡهِمۡ لَوۡ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِهِمۡ عَلِيمًا ٣٩
Wamādhā 'alayhim law āmanū billāhi wal-yawmil-ākhiri wa anfaqū mimmā razaqahumullāhu wakānallāhu bihim 'alīmā
Na ingeli wadhuru nini wao lau wangeli muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema. 39
Maelezo ya chini
39 Ama wamelaanika watu hawa! Kingewadhuru nini wao lau kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Akhera, na wakatoa katika alicho wapa Mwenyezi Mungu kwa kufuatana na Imani hii, na usafi wa niya, na kutaraji thawabu kama ilivyo wajibikia? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kwa ujuzi kaamili mambo yote yaliyo wazi na yaliyo fichikana ndani.