Surat An-Nisa, aya 38

4:38

وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَهُۥ قَرِينٗا فَسَآءَ قَرِينٗا ٣٨

Walladhīna yunfiqūna amwālahum ri'ā'an-nāsi walā yu'minūna billāhi walā bil-yawmil-ākhiri waman yakunish-shaytānu lahū qarīnan fasā'a qarīnā

Na ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu, wala hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho; na yule ambaye Shet'ani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya mno. 38

Maelezo ya chini

38 Na Mwenyezi Mungu hawapendi wanao toa mali kwa ajili ya kuonekana na watu, wapate kuwasifu na kuwatukuza, na ilhali wao si wenye kumuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Malipo. Kwani hao wamemfuata Shetani naye amewapoteza. Na mwenye kuwa rafiki yake ni Shetani basi ana rafiki mbaya kweli.