Surat An-Nisa, aya 35

4:35

وَإِنۡ خِفۡتُمۡ شِقَاقَ بَيۡنِهِمَا فَٱبۡعَثُواْ حَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهِۦ وَحَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصۡلَٰحٗا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيۡنَهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرٗا ٣٥

Wa in khiftum shiqāqa baynihimā fab'athū hakamam min ahlihī wahakamam min ahlihā in yurīdā islāhan yuwaffiqillāhu baynahumā innallāha kāna 'alīman khabīrā

Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari. 35

Maelezo ya chini

35 Pindi pakitokea kukhitalifiana baina ya mke na mume, na mkakhofia kutokea kufarikiana kutako leta t'alaka, chagueni waamuzi wawili. Mmoja kutokana na upande wa mume na mwengine upande wa mke. Wakitaka kusuluhiana Mwenyezi Mungu atawawafikisha wafikilie lilio kheri kwa wote wawili, nako ama kukaa kwa wema au kuachana kwa ihsani. Hakika Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu cha waja wake, kilicho dhihiri na kilicho fichikana.