Surat An-Nisa, aya 26

4:26

يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمۡ وَيَهۡدِيَكُمۡ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَيَتُوبَ عَلَيۡكُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ٢٦

Yurīdullāhu liyubayyina lakum wayahdiyakum sunanal-ladhīna min qablikum wayatūba 'alaykum wallāhu 'alīmun hakīm

Mwenyezi Mungu anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za walio kuwa kabla yenu, na akurejezeni kwenye ut'iifu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima. 26

Maelezo ya chini

26 Mwenyezi Mungu anataka kukuwekeeni wazi njia yenye maslaha kabisa, na akuongoeni kwenye nyendo njema za walio kuwa kabla yenu, na akurejesheni kwenye njia ya ut'iifu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua vyema mambo yenu, ni Mwenye kupanga baraabara katika hukumu zake kwa yanayo silihi mambo yenu.