وَكَيۡفَ تَأۡخُذُونَهُۥ وَقَدۡ أَفۡضَىٰ بَعۡضُكُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ وَأَخَذۡنَ مِنكُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا ٢١
Wakayfa ta'khudhūnahū waqad afdā ba'dukum ilā ba'din wa akhadhna minkum mīthāqan ghalīzā
Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti? 21
Maelezo ya chini
21 Na vipi ikufalieni nyinyi kutaka kurudishiwa mahari mliyo kwisha yatoa, na hali mlikwisha changanyika nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wakafungamana nanyi kwa agano lenye nguvu ambalo kwalo Mwenyezi Mungu amewajibisha muingiane nao kwa ndoa.